Top News

Friday, October 11, 2013

MAAJABU: Kontena lakutwa na shehena la Vikarogosi pamoja na viungo vya Binadamu kutoka china Vikisadikiwa ni vya dini za Masheteni


17
Wengi walioipata hii taarifa wanashangaa imekuaje ni viungo tu vya binadamu vimepatikana kwenye kontena zima vikiwa vinaingizwa Kenya? vinakwenda wapi? kazi yake ni nini?
Taarifa iliyoripotiwa na Citizen TV Kenya inasema Shehena hii iliyokamatwa baada ya kupitishwa kwenye bandari ya Mombasa inasemekana imesafirishwa na Mwanasiasa maarufu ambae kabla ya kukamatwa alisema ilikua na bidhaa za nyumbani ambapo ilipofika kwenye kituo cha ukaguzi wa mashehena cha Changamwe ilipatikana na vikaragosi vya mafuvu na mifupa ya binadamu ndipo amri ikatoka kontena likamatwe.
Baadhi ya mifupa ya binadamu iliyopatikana ni pamoja na mafuvu, miguu na mikono pamoja bidhaa za nyumba ambapo vyote kwa pamoja vilikua vinasafirishwa ambapo Afisa wa maswala ya Uhusiano mwema wa KRA Fatuma Yusuf  alithibitisha kwamba hii shehena iliingia kutoka China siku ya pili ya October 2013 kabla ya kugundulika ilikua na vikaragosi vya kutisha ikiwemo mifupa ya binadamu.
1Mpaka sasa uchunguzi wa shehena hili unaendelea lakini baadhi ya wakazi wa Mombasa wameonyesha wasiwasi wao na kusema kuna haja ya Serikali kutoa ripoti ya ibada za kishetani ambayo inasemekana kubuniwa na Rais Mstaafu Daniel Arap Moi miaka kadhaa iliyopita.
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16

2 comments :

  1. Bila shaka ni za waabudu shetani!! Hatua gani zitachukuliwa wakati wahusika ndo hao hao wanaosimamia sheria tena viongozi waandamizi serikalini! acheni tu nyie mtajitafutia majanga bure.

    ReplyDelete
  2. Mpieni Mzee Moi Vitu vyake acheni kuchunguza mali za watu.. wanajua wanakozipeleka hao waabudu mashetani.. in Jesus name Pepo TOKA.

    ReplyDelete

Designed By ApexbnewZ