Top News

Thursday, April 4, 2013

MAKALA YA STEVEN CHARLES KANUMBA MWAKA MMOJA BAADA YA KIFO CHAKE


April 7 2012 ni siku Steven Kanumba aliyofariki. Katika kuadhimisha  mwaka mmoja  tangu kifo chake Watanzania kutoka sehemu mbalimbali watakutana Leaders Club kwa lengo la kumuenzi na kuangalia yale aliyofanya katika enzi za uhai wake pamoja na Uzindizi wa Filamu yake ya Mwisho.

Hii ni Filamu itakayoziduliwa na Jacklen Wolper katika Kumuenzi Steven Kanumba
Kabla ya kifo chake Kanumba alikua amesaini mkataba ambao ungemfanya awe staa mkubwa kuliko wote Afrika Mashriki. Meneja wake wakimataifa Prince Richard ambaye ni mzaliwa wa Ghana alisema kuwa mkataba wake ungemfanya Kanumba Aigize filamu tatu kubwa

Filam ya kwanza iIitwa Bleeding Sunshine na trail ilifanyika Accra mwezi October mwaka jana. Filam hiyo ingefanyika Accra Misri na Dubai, Japo haikujulikana angeigiza uhusika gani angekua mtanzania wa kwanza Filam zaHollywood na angeigiza na mastaa wakubwa wane wa marekani
Filamu hiyo ingezinduliwa Marekani, Canada,Uingereza, Afrika Kusini,Ghana, Nigeria na hatimaye Tanzania

Katika Filamu ya Pili alikua Aigize Filamu ya Hollywood iitwayo President’s First Love akishirikiana na Rose Ndauka Pamoja na Lusy Komba Filamu hiyo kuhusu kiongozi wa Afrika Ingefanyika nchini Ghana kuanzia July na August  mwaka Jana

Filamu ya tatu ni Charity ambayo ingeanza kushutiwa April 14 nakumuhusisha pia muigizaji Lucy Komba. Tarehe ya kuigiza Filamu hiyo ilingiliana na mwaliko aliokua ameupata kutoka kwa tamasha la Filamu la San Fransisco Marekani, Huko alitakiwa kwenda kuzungumza uwezekano wa Bongo Movies kuonyeshwa kwenye Tamasha la mwaka huu, 2013. Bahati mbaya kifo kilimwita

Haya ni baadhi ya matukio ya picha Yalio katika Filamu Yake Ya mwisho Itakayo Zinduliwa 7/4/2013 Leaders Club

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ